Jumuiya ya kuwasaidia Wazanzibari

Sisi ni Jumuiya kutoka Ujrumani. Tunataka kuwasaidia Wazanzibari maskini kupata maendeleo. Kwa mfano tunataka kuwasaidia Wazanzibari kuanzisha miradi ambayo inaweza kuwasaidia kujiweza au kujiendesha kimaisha. Pia watu maskini wanaweza kupata msaada wa kusoma na watu wagonjwa wanaweza kupata msaada wa matibabu. Jumuiya yetu ina wanachama Wajerumani na Wazanzibari. Lengo letu ni kushirikiana ili tuweze kuwasaidia watu wengi kupata maisha bora.
Bado sisi ni Jumuiya mpya na bado hatuna uwezo mkubwa kuwasaidia watu wengi sana. Lakini tumeshachangia pesa za kutosha kuanzisha miradi kadhaa na tunatumaini kukua ili tuweze kuwasaidia watu wengi zaidi ambao wamekwama kimaisha kutokana na hali duni ya kimaisha.
Miradi ambayo tumeshaianzisha ni kama yafuatayo:
Tumemsaidia mzee Buheti kufanya operation katika hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar na baadaye kuendelea na matibabu ya rufaa katika hospitali za Ocean road na Muhimbili mjini Dar es Salaam.
Tumemsaidia Shehe kuendelea na masomo yake baada ya kufiwa na baba yake. Baba yake Shehe alifariki katika ajali ya meli iliyotokea 11/09/2011. Shehe anasoma pharmacist katika college of health Mbweni Zanzibar.
Tumemsaidia Kassim kuanzisha mradi wa tour huko Pemba. Madhumini ya mradi huu ni kwa kufanya matembezi wageni ya nchi kavu na baharini kwa usafiri wa baisikeli na boti.
Tumemsaidia Fatma kusoma kompyuta.
Tumemsaidia  Nuhu kuezekwa nyumba yake.
Tumemsaidia Khairat kujifundisha ushoni wa nguo.
Tumemsaidia Akama kupata matibabu.
Tumemsaidia Fatma kumlisha mtoto wake mchanga.
Tutajitahidi sana tena sana sana ili tuweze kuwasaidia watu wengi zaidi. Ukitaka kushiriki Jumuiya yetu na kuchangia au ukitaka kuomba msaada unaweza kutuandikia ujumbe wa email au ujumbe wa facebook.
Email: Info@hilfefuersansibar.de
Facebook: Hilfe für Sansibar e.V.
Kwa kufanya makosa ya lugha ya Kiswahili tunaomba msamaha. Tunaomba tuandikie na kusahihisha makosa yetu.
Ahsante.